Kuwekeza Katika Maisha ya Watu wa Kenya
Date Published
Jul 30, 2020
Authors
Mihir Prakash, Samantha Custer, Bryan Burgess, Divya Mathew, Mengfan Cheng, Rodney Knight
Publisher
Citation
Prakash, M., Custer, S., Burgess, B., Mathew, D., Cheng, M. and R. Knight. (2020). Kuwekeza Katika Maisha ya Watu wa Kenya: Kuthamini Manufaa ya Uhusiano Kati ya Marekani na Kenya. Williamsburg, VA: AidData at William & Mary.
Abstract
This report is also available in English. Ripoti hii inapatikana pia kwa Kiingereza.
Marekani ni mshirika muhimu katika azma ya Kenya ya kutimiza Ruwaza yake ya 2030, lakini ni taarifa chache ambazo Wakenya wanaweza kupata ili kuwawezesha kutathmini thamani ya ushirikiano huu katika maisha yao ya kila siku. Ripoti hii inachunguza faida za ushirikiano kati ya Kenya na Marekani katika ukuaji na ustawi wa Kenya kwa msingi wa mtazamo wa jamii nzima. Kwa pamoja, mawakala wa serikali ya Marekani, mashirika na watu binafsi huchangia takriban Dola bilioni 3.05 kila mwaka (KSH B 310) katika maendeleo ya Kenya.
Mbali na faida hizi za kifedha, ushirikiano wa Kenya na Marekani huchangia katika ukuaji na ustawi kupitia njia nyingine zinazoweza kuonekana. Msaada wa Marekani unaolenga afya hausaidii tu kuokoa maisha ya watu, bali pia unachangia katika uzalishaji wa kiuchumi wa Kenya kadiri watu wanavyoendelea kufanya kazi kwa muda mrefu zaidi. Kama mtoaji mkubwa zaidi wa fedha zinazohusiana na HIV/UKIMWI (Dola bilioni 4.5 kati ya 2009-2018), Marekani imehamasisha rasilimali na utaalamu wa kusaidia wafanyakazi wa afya wa mstari wa mbele katika juhudi zao za kupambana na janga la UKIMWI. Tunakadiria kuwa juhudi hizi zimesaidia kuokoa maisha ya watu zaidi ya milioni moja hadi kufikia leo.